Serikali imeendelea kutenga fedha za ukarabati wa shule chakavu nchini zikiwemo shule za msingi katika Vijiji vya Kalundi, Lyapinda na Londokazi kadri ya upatikanaji wa fedha.
Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anyeshughulikia Elimu, Zainab Katimba wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Nkasi Kusini, Vicent Mbogo aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuhusu ukarabati wa Shule za Msingi katika Vijiji vya Kalundi, Lyapinda na Londokazi vilivyopo katika jimbo hilo.
Akijibu swali hilo Katimba amesema, “kuanzia mwaka 2022/23 hadi 2023/24, Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya ukarabati, ambapo shilingi bilioni 70.39 zimetolewa kwa ajili ya ukarabati wa shule 793 zikiwemo Shule za Msingi Chalantai, Nkundi na Sintali za Jimbo la Nkasi Kusini” amesema.
Aidha, amesema serikali katika mwaka wa fedha 2024/25 imetenga fedha kwaajili ya ukarabati wa shule kongwe na chakavu hatua inayoendelea ni kutathimini na itakapokamilika serikali itaweka kipaumbele kwenye shule yenye miundombinu chakavu.

Malimwengu: Miwani ya kubaini uongo yavunja ndoa 100
Nafasi Makamu wa Rais Kenya: Kindiki kuapishwa leo?