Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Serikali Nchini, imewahakikishia Wananchi kuwa itaendelea kutoa ushirikiano kwa Kanisa Katoliki na kuhakikisha Ustawi na waumini wote unaimarika na mshikamano kuendelezwa.
Salamu hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga kwa niaba ya mgeji rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Misa Takatifu ya Kutabaruku Kanisa la Roho Mtakatifu Parokia ya Babati.
Katika Misa hiyo ya luwekwa Wakfu na kulitakasa kwa ajili ya Maadhimisho Matakifu na pia waimarishwa zaidi ya 200 wamepokea Sakramenti ya Kipaimara yaani wamefanywa kuwa imara Askari hodari wa yesu Kristo,Misa ambayo imeongozwa na Mhasham Askofu Anton Lagwen wa Jimbo Katoliki la Mbulu.
Sendiga amesema, Rais Samia amemuagiza kuwakumbusha waumini wa Kanisa Katoliki kujitokeza kwa wingi November 27 kupiga kura ya kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa, vijiji na vitongoji huku akiwaomba kwa nafasi zao kutoa hamasa kwa wengine kujitokeza kwakua ni haki yao kikatiba.
Amesema, “ameushukuru Mkoa wa Manyara kwa kuandikisha Zaidi ya wanachi laki 8 sawa na asilimia 90,hivyo matarajio yake wanachi wote hao waliojiandikisha watakwenda kupiga kura na kuchagua Viongozi wao wa Serikali za Mitaa, vitongoji na vijiji.”
Aidha, Sendiga ameahidi kuwa Uongozi wa Mkoa pamoja na Serikali kuu kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha na kuwa na upendo ili kuhakikisha Ustawi wa wananchi wa Manyara unimrika.
Awali, wakati wa Misa hiyo Mhasham Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu, Anton Lagwen amewaalika waamini wa Kanisa hilo kujiombea na kuwaombea waimarishwa hao pamoja na familia zote kwa lengo la kupingana na adui wa roho ili kujiepusha kuingia katika matendo yasiofaa.
“Maadui wa roho ni wengi sana,ibilisi ni adui wa roho,tabia yangu mbaya ni adui wa roho,watu wabaya na wenyewe ni adui wa roho hasa wao wanakwamisha kwenye masuala ya Imani lakini pia mazingira yasiyoafaa ambayo unaweza ukajitumbikiza ni adui wa roho,” alisema.
Imeelezwa kuwa Kanisa la Roho Mtakatifu Parokia ya Babati ambalo limejengwa kwa miaka 11 huku Rais Samia alichangia ujenzi huo kwa Shilingi milion 100 na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali.