Muigizaji Nguli Nchini, Grace Mapunda ‘Tesa’ ambaye amekuwa akionekana kwenye tamthilia ya Huba amefariki Dunia.
Grace ambaye amejizoea umaarufu kupitia fani yake hiyo ya uigizaji, amefariki asubuhi ya leo Novemba 2, 2024 akiwa anaendelea kupokea matibabu katika Hospitalini ya Mwanayamala iliyopo jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na watu kadhaa wa karibu yake akiwepo Muigizaji Idris Sultan na Director Aziz Ahmed ambaye alikuwa akifanya naye kazi kwa ukaribu akisema ni kweli Grace ametangulia mbele za haki.
Amesema, “ni kweli amefariki usiku wa kuamkia leo Mwananyamala Hospitali. Hajaumwa muda mrefu aliletwa Hospitali juzi (Oktoba 31, 2024) kisha jana tukaja kumuona ila usiku wa kuamkia leo (Novemba 2, 2024) ndio hivyo tena.”
Grace Mapunda, atakumbukwa kwa mchango mkubwa kwenye Tasnia ya uigizaji, akivaa uhusika mbalimbali na msiba uo nyumbani kwake Sinza Vatican.
PUMZIKA KWA AMANI GRACE MAPUNDA.