Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, limewataka Wananchi wa Kata ya Itebula Wilayani Uvinza kutojichukulia Sheria mkononi, ikiwemo kuwashambulia watuhumiwa wa jinai na badala yake wawafikishe vituo vya Polisi kwa hatua za kisheria.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Nguruka, Mrakibu msaidizi wa Polisi Ezekiel Mayani wakati akitoa elimu ya utii wa sheria kwa Wananchi hao.
Amesema, watuhumiwa wa makosa ya jinai wanapaswa kufikishwa vituo vya Polisi, ili upelelelezi ufanyike na baadae kufikishwa Mahakamani kwa hatua za kisheria.
ASP Mayani amebainisha kuwa, vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kuwashambulia watuhumiwa wa jinai hupelekea majeruhi, vifo na hata uharibifu wa mali.