Dani Olmo aliifungia Barcelona mabao mawili katika mechi yake ya kwanza baada ya kurejea kutoka majeruhi. Barcelona waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Espanyol siku ya Jumapili. Matokeo hayo yamewafanya Barca kukaa kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa utofauti wa alama 9.
Klabu ya Real Madrid inashika nafasi ya pili ikiwa haijacheza mchezo wao dhidi ya Valencia baada ya kusitishwa mchezo huo kwa sababu ya mafuriko makubwa katika eneo hilo,
Katika mchezo wa Barcelona dhidi ya Espanyol kikosi cha Hansi Flick kilinyoosha uwezo mkubwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa mchezo wakijitanabaisha kuutaka ubingwa wa La Liga msimu hu.
Kiungo mshambuliaji Raphinha alipachika wavuni bao moja katika mchezo huo na kumfanya aweze kufikisha mabao 7 katika mechi 12 za La Liga msimu huu. Winga huyo wa kushoto amekuwa tishio kwa sasa baada ya kufunga mabao 11 katika michezo 15 aliyocheza msimu huu.
Kurejea kwa Dani Olmo na kufunga mabao mawili kunamfanya kocha Hansi Flick kuendelea kuwa na kikosi kipana chenye wachezaji bora wenye kushindana.Uwepo wa Frank De Jong,Gavi ,Pedri na Dani Olmo kunampa wasaa mzuri kocha huyo kufanya machaguo sahihi kwa kila mchezo.