Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Agustivo iliyopo Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, wametakiwa kuepukana matendo vya kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi, ili waweze kuepukana na mimba za utotoni zitakazowaharibia masomo pamoja kutotizimiza ndoto zao.
Hayo yamesemwa hii leo Novemba 6, 2024 na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Ally Alijai akiambatana na Watendaji wa Dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Mbinga ambao ni Koplo Asia na Koplo Debora.
Askari hao waliptembelea shuleni hapo kwa lengo la kutoa elimu ua ukatili wa kijinsia na madhara yake, ikiwa ni muendelezo wa Kampeni ya tuwaambie kabla hawajaaribiwa.
Pamoja hilo Koplo Asia amewataka Wanafunzi hao kuhakikisha wanatambua wajibu wao pindi wanapokuwa shuleni na nyumbani kwa kutojihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili kama vile mapenzi ya Jinsia moja.