Mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump anayewania kinyang’anyiro cha kuingia katika Ikulu ya White House dhidi ya mgombea wa mgombea wa chama cha Democratic, Kamala Harris amejitangazia ushindi, licha ya kuwa bado hajapata kura rasmi zinazohitajika za wawakilishi maalum wanaopiga kura kumchagua rais wa Taifa hilo.

Trump ametangaza hatua hiyo wakati akiwahutubia wafuasi wake  na kusema sasa itakuwa “zama za dhahabu” kwa Taifa la Marekani, huku na baadhi ya viongozi wa dunia wakianza kumpongeza akiwemo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Mwingine ni Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban ambaye kupitia mtandao wa kijamii ametoa pomngezi kwa kuandika kuwa,  “Trump amerejea kwa kishindo katika historia ya kisiasa ya Marekani! Hongera Rais Donald Trump kwa ushindi wake mkubwa.”

Hata hivyo, Trump amejitangazia kupata ushindi – lakini bado hajafikia idadi ya 270 ya kura za wawakilishi maalum zinazohitajika kutoka kwa Wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchaguzi nchini Marekani inamchagua Rais, maarufu kama Electoral College.

Dkt. Mpango ashiriki mazishi ya John Tutuba
Bungeni: Serikali imesajili miradi 63 ya biashara ya Kaboni