Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Serikali Nchini, imetoa ruzuku ya Mbegu bora ya Mahindi kwa Wakulima ikiwa na lengo kuleta mageuzi na tija kwenye Sekta ya Kilimo, ili kuweza kumnufaisha mkulima kwa kupata uhakika wa chakula katika ngazi ya kaya na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ameyasema hayo alipokua akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake na kuwataka wakulima kuichangamkia fursa hiyo vizuri kwa kununua mbegu bora za mahindi kwa bei nafuu kutoka kwa wauzaji ili kuongeza uzalishaji wenye tija.
Amesema, “Mbegu bora ya Mahindi imefungwa katika uzito wa kilo mbili mbili kwa Shilingi elfu 14 ambapo awali mbegu hii ilikua inauzwa Shilingi elfu 18,19 mpaka 20 na nyingine zaidi ya hapo kulingana na muuzaji anavotaka, lakini Serikali imekwisha toa muongozo,lakini pia kuna mbegu zinazochavushwa,izo mbegu likua zinauzwa kati ya elfu 10,15 na kuendelea ,hizo kwa bei ya ruzuku zitauzwa Shilingi elfu 7 kwa Mfuko wa kilo 2.”
Sendiga ameongeza kuwa, Mkulima anapaswa kujisajili katika mfumo wa ruzuku ambao unatambulika tangu awali ili Kila mmoja aweze kupata manufaa na kuwaasa wakulima kujitokeza kujisajili kwa wingi na kuacha kusikiliza watu wenye nia ovu ya kuwakatisha tamaa wasiweze kupata ruzuku hiyo.
Aidha, ametoa maelekezo kwa waagizaji,wasambazaji na mawakala ambao wamejisajili wahakikishe kwamba mbegu hizo za ruzuku ziuzwe na kwa bei elekezi na kuitaka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara inayoshughulikia Kilimo na Uchumi kuhakikisha kwamba wanapunguza changamoto ya kupata mbegu hizo kwa Wakulima waliopo maneno ya mbali.
“Fedha ambayo imepunguzwa kwenye hii mbegu,wakulima waweze kuipata na waifurahie manake tusipolitekeleza hilo tutakua tunamrudisha mkulima pale pale nyuma kwenda kufata mbegu yake mbali na akatembea Tena kurudi mbali matokeo yake kile kiasi Cha fedha ambacho Serikali imekusudia mkulima aweze kukisevu pengine hakitoonekana.”
Naye,Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Manyara Faraja Ngerageza anayesimamia Uchumi na Uzalishaji amesema Mkoa umesajili Zaidi ya wakulima elfu 80 wa ruzuku ya mbolea ambapo mfumo huo pia utatumika kusajili wakulima wa ruzuku ya mbegu bora ya Mahindi.
“Kilio Cha watu wengi ilikua wanataka tuweke ruzuku pungufu ya bei kwaajili ya mbegu,sasa muheshimiwa Rais akasikia Sasa ndo maana tumeanza na hiyo mbegu kwanza,mana mwingine kwenye mbolea anakwambia Mimi natumia sana samadi”.
Kwakua Kilimo ni Uti wa Mgongo Nchini, Serikali imeamua kuendelea kuboredha Sekta ya Kilimo na kutaka kujihakikishia kwamba Kila Mtanzania ananufaika ambapo katika mwaka huu wa fedha imeongeza takriban Shilingi Trillion 91 fedha ambazo zinasaidia kufanya maboresho mbalimbali ikiwemo kutoa ruzuku za pembejeo za kilimo pamoja na kununua vitendea kazi.
Juhudi hizo za kufanya maboresho kwenye Sekta ya Kilimo, zinaendelea kumsaidia kwa kumpungizia mkulima mzigo mzito na majukumu ya kutekeleza Kilimo kwakua atatumia kilimo Cha kisasa ambapo kitampa tija, kwani Nchi chache za Afrika zimekuwa zikitoa ruzuku za pembejeo za kilimo kwa wakulima ambapo kwa mara ya kwanza utolewaji wa ruzuku hizo umefanyika Nchini.