Liverpool wanajiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua kiungo wa Real Madrid Aurelien Tchouameni, Manchester United kufufua nia yao ya kumnunua beki wa Everton Jarrad Branthwaite na Arsenal wafanya mazungumzo na mshambuliaji wa Sporting Geovany Quenda.

Liverpool wanaandaa dau la pauni milioni 50 kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 24. (Fichajes – kwa Kihispania)

Juventus wanamtaka mshambuliaji wa Lille Jonathan David, lakini klabu hiyo ya Serie A inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester United, Liverpool na Arsenal kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Canada mwenye umri wa miaka 24. (Corriere dello Sport – kwa Kiitaliano)

Manchester United wamefufua tena mpango wa kumnunua beki wa Everton mwenye thamani ya pauni milioni 70, Jarrad Branthwaite, huku klabu hiyo ya Merseyside ikishindwa kumudu kandarasi mpya kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 22. (Mail – usajili unahitajika)

Brighton na Bayer Leverkusen ni miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa na beki wa Red Star Belgrade Mserbia Strahinja Stojkovic aliye na umri wa miaka 17. (Football Insider)

Arsenal wamefanya mazungumzo na mawakala wa shambuliaji wa Sporting Geovany Quenda, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 pia akiwaniwa na na Manchester United, Manchester City na Liverpool. (Team Talk)

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 36, yuko tayari kupunguziwa mshahara ili kusalia Barcelona na kiwango chake kizuri kimeifanya klabu hiyo ya Catalan kupoza hamu ya kumnunua mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland, 24, kutoka Norway. (Sport – kwa Kihispania)

AC Milan wako tayari kuongeza mara mbili mishahara ya kiungo wa Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, asinyakuliwe na Manchester City na Tottenham. (Calciomercato – kwa Kiitaliano)

Manchester City wanamfuatilia kiungo wa kati wa Inter Milan Hakan Calhanoglu, 30, ingawa Bayern Munich wako katika nafasi nzuri ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki. (Caughtoffside)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta atakuwa na uamuzi ni nani kuchukua nafasi ya Edu kama mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo baada ya Mbrazil huyo kuamua kuachana na The Gunners. (Times – usajili unahitajika)

West Ham wanaamini kwamba mkurugenzi wa ufundi Tim Steidten anaweza kuzingatiwa na Arsenal kama mbadala wa Edu. (Telegraph – usajili unahitajika)

Arteta

Chanzo cha picha,Getty Images

Beki wa Tottenham Cristian Romero huenda akahamia Real Madrid msimu huu wa joto ikiwa klabu hiyo ya La Liga itaimarisha mpango wa kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 26. (GiveMeSport – usajili unahitajika)

Paris St-Germain wako tayari wamefutilia mbali uhamisho wa mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 26, licha ya ufungaji mabao wake mahiri katika klabu ya Sporting. (Le Parisien – kwa Kifaransa)

Arsenal bado wanavutiwa na mshambuliaji wa RB Leipzig raia wa Slovenia Benjamin Sesko, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akiwa na kipengele cha kumnunua cha £55m katika mkataba wake. (Mail – usajili unahitajika)

Sesco

Chanzo cha picha,Getty Images

Mkufunzi wa Wolves Gary O’Neil huenda akafutwa kazi ikiwa timu yake haitaifunga Southampton katika mechi ya Ligi ya Premia wikendi hii. (Telegraph – usajili unahitajika)

Paris St-Germain wako tayari kumruhusu mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 25, kuondoka mwezi Januari huku klabu za Ligi ya Premia na Bundesliga zikiwa tayari kumnunua. (RMC Sport – kwa Kifaransa)

Manchester United yarejea kwa kishindo Europa
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 8, 2024