Serikali Nchini Australia inatarajia kuwasilisha Bungeni muswada wa sheria utakaopiga marufuku matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16.

Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese amesema kuwasilishwa kwa muswada huo kunatokana na ukweli kuwa mitandao ya kijamii inaharibu watoto na kwamba Serikali yake imedhamiria kuwalinda.

Amesema, iwapo sheria hiyo itapitishwa na Bunge itaanza kutumika katika kipindi cha miezi 12 inayokuja na itayalazimisha makampuni ya mitandao ya kijamii kusaidia utekelezaji wake.

Mapendekezo hayo, yanakuja wakati Serikali ulimwenguni zinapambana kutafuta njia za kusimamia au kudhibiti matumizi ya teknolojia katika simu mamboleo na mitandao ya kijamii kwa Vijana.

Elimu ya mpiga kura kutolewa kwa makundi yote - INEC
Ustawi wa Taifa: Viongozi timizeni majukumu yenu - Mchengerwa