Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amezindua rasmi programu ya upandaji wa miti ya Michikichi katika Mto Mpiji kwa lengo la kurejesha uoto wa asili na kuthibiti mmomonyoko wa udongo na kuimarisha mazingira yanayoathirika zaidi kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Hafla hiyo ya uzinduzi imewakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira wakiwemo NEMC, Wakandarasi pamoja na vikundi cha Machepe ambapo jumla ya Miti ya Michikichi 5,000 imepandwa katika eneo hilo itakayokwenda kuhifadhi mazingira lakini kuwa chanzo cha mapato kwa wananchi wa maeneo hayo.

Akizungumza na Wananchi, Chalamila amesisitiza suala la utunzaji wa mazingira hususani chanzo hicho cha maji na kuiagiza Wami/Ruvu kuweka uangalizi wa karibu na ufuatiliaji wa Miche hiyo iweze kuleta tija na kutimiza malengo yaliyowekwa kwa Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Awali, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy ameeleza lengo la kupanda michikichi katika eneo hilo ni kuleta uhifadhi wa mazingira shirikishi ili wananchi watunze mito huku wakinufaika na mafuta ya miti hiyo.

“Michikichi kwa uhifadhi wa mazingira na uchumi endelevu “

Babati: Wizara iharakishe mchakato makubaliano uzalishaji Mbolea asili
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 11, 2024