Boniface Gideon –  Tanga.

Mjasiriamali na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mdari Athumani ambaye ni mkazi wa Duga Jijini Tanga, ameiomba Serikali na Viongozi wa Mkoa huo kumsaidia mtaji wa Biashara baada ya kukumbwa na hali ngumu ya kifedha kufuatia Mke wake kumwibia Shilingi Milioni 10 na kutokomea kusikojulikana.

Akizungumza na kituo hiki hii leo Novemba 12, 2024 Hussein amesema fedha zilizoibwa na mkewe alikopa Benki kwa ajili ya kuendeleza biashara zake, lakini amepoteza mweklekeo baada ya mkewe huyo kufanya uhalifu na kumrudisha nyuma kiasi ameshindwa kusimamia biashara hiyo.

Amesema, “naomba msaada kutoka kwa serikali yangu ya Mkoa wa Tanga, pamoja na viongozi wangu wa chama cha siasa, hususan Mwenyekiti wa Mkoa, Mheshimiwa Abdallahman Rajab ili niweze kuinuka tena na kuendelea na shughuli zangu za kimaisha, hasa kuwahudumia watoto wangu ambao mke wangu aliniachia baada ya kutoroka na fedha milioni kumi.”

“Ninaamini kupitia Serikali yangu ya Mkoa ,inayoongozwa na Dkt. Batilda Burihani, na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Ndugu Japhari Kubecha, wanaweza kunisaidia kwa namna moja au nyingine ili niweze kujikwamua na kurejesha hali yangu ya kifedha,” amesema Hussein.

Mjasiriamali huyo, ameongeza kuwa, “kwa sasa Benki inamdai na wanataka kuuza Nyumba aliyojenga kwa ajili ya familia yake ili kufidia deni. Hali yangu ni mbaya, lakini bado naimani kuwa msaada utapatikana. Hata Mheshimiwa Ummy Mwalimu aliguswa na shida yangu na kunilipa kodi ya fremu ya biashara. Namshukuru sana kwa msaada wake,” alisema Hussein.

Hussein ambaye anasema taarifa za wizi huo tayari alikwisha ziripoti Polisi licha ya kuwa mtuhumiwa bado hajakamatwa, pia alitumia fursa hiyo kuomba msaada kutoka kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, akisema, “nikiwa kada wa chama cha Mapinduzi, naomba msaada wa dhati kutoka kwa viongozi wangu, ili niweze kusimama tena na kumudu maisha yangu.”alisisitiza Hussein

Muleba: Madiwani waishukia TANESCO Visiwa 13 kukosa Umeme
Polisi: Vijiwe vitumike kupeana maarifa kimaisha si uhalifu