Daraja la Muhoro ambalo hivi sasa linasukwa kwa ustadi kumbwa na wa hali ya juu lilinatarajia kutoa fursa kwa watanzania kufanya shughuli zao kwa ufanisi baada ya kukamilika kwake, ambapo pia Watanzania wataweza kusafirisha bidhaa zao ikiwemo mazao kwa ajili ya kujiingizia kipato.
Daraja hilo, litaweza kuingiza watalii kwa wingi kutokana na kwamba watakuwa wanauwezo wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa urais zaidi tofauti na mwanzo ikizingatiwa eneo la Mbwela lina bichi mzuri sana kwani ni pembezoni mwa bahari ya Hindi ambapo maeneo hayo hayatumiki kwa sasa kutokana na kutokuwepo barabara na daraja hilo na baada ya hapa sasa yataanza kutumika.
Meneja Mkuu wa TARURA Pwani Rufiji, Leopold Runji amesema mara baada ya kukamilika kwa daraja hilo mazao mbalimbali kama Samaki, Maembe, Matikiti, Nanasi, Mastaferi, Mpunga, Mapapai, Machungwa, Mafenesi, Maparachichi, Nazi, Korosho, na bidhaa zingine zitapitishwa na wafanyabiashara wa Kitanzania kwa ajili ya kwenda kuuza na kujiingizia kipato.
Amesema, pia Magari, Bodaboda, watembea kwa miguu, Baiskeli, Guta, Magari makubwa nk, vyote vitatumia daraja hilo kwenye Wilaya husika, kwani awali kulikuwa mitambo ambayo ilishindwa kupita kwa ajili ya shughuli za Kilimo, miradi ya ujenzi kwa ajili ya shughuli za kilimo, ujenzi wa barabara kwa kutumia madaraja vilikuwa vikisafilishwa kwa kutumia meri au boti.
Lunji ameongeza kuwa, ujenzi huo wa daraja unaendelea vizuri katika hatua mbalimbali ambapo ujenzi wa maboksi karavati yamefikia asilimia hamsini na mawili yanaendelea kwenye ukarabati wakati ujenzi wa daraja kuu unaendelea kwa asilimia kubwa na kwamba mitambo inatengenezwa na kusukwa kwa asilimia sitini na kwamba mpango kazi ni kukamilisha kwa ndani ya muda wa wa mkataba.
Naye Mhandisi Mkazi Emmanuel Mahimbo kutoka TREECO-Pwani katika Daraja la Mohoro, amesemwa daraja hilo linaendelea vizuri kutokana na kwamba watendaji wanafanya vizuri na wanajituma katika kuhakikisha kazi inatimia kwa wakati.
Amesema, “Nipende kusema kuwa tuko vizuri katika utekelezaji wa jambo hili ambalo ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, kwani naamini baada ya hapa hakuna mwananchi atakayeweza kulalamika. “Lakini nipende kuweka wazi kuwa Teknojia inayotumika haina kiswahili badala yake inaitwa (CFA) Continuase Flaith Auge, ambapo vyovyote itakavyokuwa mvua ikinyesha hakuna cha kuendelea ila kinachotakiwa ni kumaliza kabla ya mvua hazijanyesha.”
Aidha, alisema kutokana na mpango huo wa Mhandisi Mshauri na Mkadarasi ambao wamejipanga vizuri matarajio yake ni kwamba kabla ya mvua hizo kuendelea chini ya daraja patakuwa pamekamilika kumaliza na kukamilika kwa wakati.
Hata hivyo, amebainisha kuwa kama Taasisi wanayo matarajio ya kuongeza pato la Serikali kupitia kwa Rais Samia Suhuhu Hassan, kutokana na jinsi alivyowezesha miradi hiy na sasa wanaamini kuwa Wananchi wana matumaini ya kuwa na maendeleo makubwa.