Mwanamuzi nguli wa Dansi Nchini, Boniface Kikumbi Mwanza Mpango maarufu kama King Kikii amefariki Dunia usiku wa kuamkia hii leo Novemba 15, 2024 akiwa na umri wa kiaka 77.

Kwa mujibu wa Mtoto wake Joseph Kikumbi ambaye amezungumza kwa njia ya simu amesema Baba yake amefariki majira ya saa saba na nusu usiku baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani.

 

Amesema, “Mzee alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali kama unakumbuka lakini wiki mbili zilizopita akiwa Muhimbili tuliomba ruhusa kurudi nyumbani kutokana na hali yake na mpaka anafariki alikuwa akiugua tezi dume na Kansa ya ini.”

Msiba wa Mzee King Kikii upo nyumbani kwake Mtoni kwa Azizi Ali Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo Joseph amesema wanatarajia kumpumzisha makaburi ya Kinondoni baada ya taratibu kukamilika.

Mzee King Kikii enzi za uhai wake aliwika na bendi mbalimbali ikiwemo Marquis Original, Orchestra Safari Sound – OSS wana Ndekule, Orchestra King Kikii Double O, Orchestra Sambulumaa Band, Zaita Musica na Capitale Wazee Sugu.

WHO yatoa takwimu maradhi ya Surua
Watkins afanya kweli Uingereza ikilipa kisasi kwa wagiriki