Uongozi wa klabu ya Yanga chini ya Rais Hersi Said wamekuwa na vikao vya mara kwa mara ikiwa ni kujadoli mwenendo wa timu yao baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo.

Yanga imepoteza dhidi ya Azam FC bao 1-0 limefungwa na Gibril Sillah na mechi ya pili na Tabora United kwa mabao 3-1, mechi zote zilipigwa kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi Dar-es-Salaam.

Imeelezwa kuwa baada ya mechi na Tabora United kamati ya utendaji ya Yanga ilikutana na kubaini mambo matano kutoka kwa kocha wao Miguel Gamondi ambaye amekalia kuti kavu huku ikidaiwa Kheireddine Madoui kutoka Algeria, aliyewahi kufundisha CS Costanteno ambaye ni wapinzani wa Simba  katika kombe la Shirikisho Afrika, kuchukuwa nafasi yake.

Gamond anatajwa kuondoshwa kutokana na vitu vingi ikiwa mwenendo mbaya wa timu kwenye mechi mbili za mwisho lakini sababu kubwa ikitajwa kuwa hashauriki, amepoteza ushawishi kwenye timu, jeuri, ubishi na kutoelewana na wasaidizi wake wengine.

“Baada ya mechi Kamati ya utendaji ilikaa vikao mara mbili cha kwanza kocha Gamond (Miguel) alitakiwa kuhudhuria lakini hakutokea, lengo kubwa la vikao hivyo kuona wapi tunapokosea na kujiweka sawa mapema.

Gamod bado yupo kwenye uangalizi, kama kutakuwa na mabadiliko yatawekwa wazi kwa sababu mapema kuongea suala la kocha mpya,”amesema chanzo cha habari ndani ya Yanga.

Amesema kocha huyo hakutokea kwenye kikoa cha kwanza lakini wanaimani watakutana naye na kuzungumzo kuona walipojikwaa na kuendelea na majukumu yake kwa uangalizi maalum kuelekea mechi yao ya Ligi ya Mabingwa.

Alipotafutwa Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema hayo ni matokeo ya mpira, akili na nguvu zetu kwenye mechi zijazo, tofauti pointi moja kwenye msimamo, bado wana mechi nyingi mbele.

“Hapa kwenye Ligi tutaparudia tunaelekeza nguvu yetu sasa namna gani tunarudi kwenye ubora wetu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, tuna wiki mbili za kufanya maandalizi makubwa sana na kurudi kwenye mapigo yetu, katika nyakati hizi ngumu ndio tunapaswa kusimama kama wananchi na kuonyesha ukubwa wetu,” amesema Kamwe.

Simba wamjia juu straika msumbufu anayetaka kuondoka
Tetesi za usajili Duniani Novemba 15