Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameongoza Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC-Organ) uliofanyika Novemba 17, 2024 jijini Harare, Zimbabwe.

Waziri Kombo ameungana na Mawaziri wenzake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) pamoja na njia mbalimbali za kurejesha amani nchini humo na kubainisha kuwa Tanzania inaunga mkono juhudi zote zinazofanyika katika kurejesha amani Mashariki mwa DRC.
Amezisisitiza Nchi za SADC kushirikiana ili kutafuta suluhu ya kudumu ya kurejesha amani Mashariki mwa Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), akisema, “ni jukumu la kila Nchi Mwanachama kushirikiana kwa pamoja katika kurejesha amani na usalama kwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).”
Viongozi wengine kutoka Tanzania walioshiriki Mkutano huo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda.
Wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Talha Waziri.

Halaand anatisha aweka rekodi nyingine Ulaya
Ajira: Waziri ashangaa idadi ndogo waombaji kazi