Klabu ya Yanga imeendelea kufanya maboresho ya benchi la ufundi baada ya kumleta Mkurugenzi mpya wa idara ya ufundi atakayesaidiana na kocha mpya Sead Ramovic. Yanga wamemtambulisha Abdi Moallin kama mkurugenzi wa ufundi akitokea KMC kama kocha mkuu wa timu hiyo.

Yanga imeendelea kuongeza nguvu katika idara zake zote kuelekea michuano ya kimataifa na ligi kuu ambapo tarehe 26 Novemba watacheza mchezo wao wa kwanza wa ligi ya mabingwa Africa hatua ya makundi dhidi ya Al Hilal mchezo utakaopigwa dimba la Benjamin Mkapa. Wengi tunautafsiri ujio wa Moallin ni katika kuimalisha benchi la ufundi ambalo lilikosa idara hiyo tangu kuondoka Van Pluijm aliyeshikilia wadhifa huo miakamichache iliyopita kuondoka.

Mara baada ya kutambulishwa rasmi Abdi Moallin amenukuliwa akisema ‘‘Nina furaha kuwa sehemu ya klabu hii,kuwa sehemu ya historia yakena kuwa sehemu ya mafanikio ya siku zijazo”

Ukiachana na ujio wa Kocha mkuu Sead Ramovic na Abdi Moallin klabu hiyo imejiandaa kunasa saini ya kocha msaidizi ambaye atatambulishwa hivi karibuni.

 

Mustafa Kodro atangazwa kuvaa viatu vya Moussa Ndauw
Lee Carsley awaaga waingereza kwa kishindo akimpa kibarua kizito Tomas Tuchell