Katika kuhakikisha Elimu inasonga mbele kwa kasi, Polisi wa Kata ya Miguruwe Wilaya ya Liwale Mkoan Lindi, Koplo wa Polisi Muhudi Machuma amewaelemisha Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Miguruwe kuhusu umuhimu wa Elimu, madhara ya mapenzi shuleni, ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia.
Koplo Machuma aliwapa elimu hiyo mara baada ya kutembelea Shuleni hapo na kuwataka Wanafunzi hao kuyapa kipaumbele masomo kuliko mapenzi na kamwe wasikubali kurubuniwa kwani wanaweza kuharibu ndoto zao kimaisha huku akiwasisitia kuridhika na wapewacho na wazazi au walezi ikiwemo kujiepusha na makundi mabaya.
Amesema, Wanafunzi hao wanatakiwa kuchukia vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto, kwa kutoa taarifa kwa Walimu au Polisi pindi wafanyiwapo au waonapo viashiria au vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili wa watoto ili kujiokoa wao na wenzao na watuhimiwa waweze kufikishwa katika mikono ya sheria.
Machuma pia aliwaeleza madhara ya kufumbia macho vitendo hivyo kuwa vinaweza kusababisha vifo, mimba za utotoni, ulemavu wa kudumu, kuambukizwa virusi vya ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa, umasikini, kufifisha malengo ya baadae ya watoto hasa Wanafunzi na visasi vinavyopelekea watu kuwa wahalifu.

Uchaguzi: Hapi kuzindua Kampeni za CCM Kagera
Maagizo mapya ya Rais Samia Jengo lililoporomoka Kariakoo