Bao pekee na muhimu lililofungwa na Simon Msuva dakika ya 61 limeiwezesha Tanzania kufuzu michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco. Ushindi huo muhimu wa Taifa Stars dhidi ya Guinea umeiwezesha Stars kufikisha alama 10 kwenye  kundi H na kushika nafasi ya 2 nyuma ya Congo DR yenye alama 12.

Kufuzu kwa Taifa stars ni hatua muhimu kwa nchi yetu tunapoandaa michuano ya CHAN2025 pamoja na AFCON2027. Hii inakuwa mara ya tatu kwa kipindi cha miaka 6 Taifa Stars kushiriki michuano hiyo ikifanya hivyo mwaka 2019,2023 na 2025.

Katika mchezo huo kocha Hemed Suleiman alianza na kikosi kilichoundwa na Aishi Manula,Shomari Kapombe,Mohammed Hussein ,Dickson Job ,Ibrahim Hamad,Mudathir Yahya,Bitegeko,Saimon Msuva,Feisal Salum,Clement Mzize na Mbwana Samatta.Kikosi hicho ndicho kilichoipa Stars ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia.

Tetesi za usajili Duniani Novemba 20
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 20, 2024