Johansen Buberwa – Kagera.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi – CCM Taifa na Mjumbe wa Sekretalieti ya Halmashari kuu, Ally Salum Hapi amesema mpaka sasa nchi ya Tanzania imepiga hatua kubwa ya kuwafikishia umeme Wananchi wanaoishi vijijini kwa asilimia 97.

Akizungumza wakati wa kuzindua Kampeni za CCM Mkoa wa Kagera hii leo Novemba 20, 2024 Manispaa ya Bukoba Hapi amesem Umeme Vijijini mpaka mwanzoni mwa mwaka huu umevifikia zaidi ya Vijiji 11,000 nchi nzima na vimebaki Vijiji 480.

Amesema, “Wagombea wa Vijiji na Vitongoji nendeni tutapeleka umeme kila nyumba ya mtanzania iwe ya bati itapata umeme iwe ya mabanzi itapata umeme yamatofari ya kuchoma umeme ya matope umeme wambie ndugu zenu wa vijijini Dkt Samia atapeleka umeme.”

Katika hatua nyingine katibu Hapi amesema Dkt Samia Hassan alikuta bwawa la mwalimu Nyerere likiwa limefikia asilimia 34 leo hii bwawa hilo limekamilikwa asilimia 99.99 na mpaka sasa kama nchi ya Tanzania tayari imesha kunufaika kwa kutumia umeme wa bwawa hilo ambapo amesema Chama hicho kina kiongozi mwenye maono anayetokana na Chama cha mapinduzi.

Wagombea wa uchaguzi wa serikali za mitaa Mkoa wa Kagera kupitia ccm kwa mwaka huu wa vijijini ni 662 na mitaa 66.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 21, 2024
Picha: Rais Samia akagua eneo la maafa ajali ya Kariakoo