Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania – TET, Dkt. Aneth Komba amesema Taasisi hiyo inatarajia kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake ifikapo Mwezi Mei 2025.
Dkt. Komba ameeleza hayo katika hafla ya uzinduzi wa usambazaji wa vitabu vya washindi wa tuzo ya Taifa ya Uandishi Bunifu iliyofanyika katika ofisi za TET Jijini Dar es Salaam.
Alisema, katika kuelekea maadhimisho ya miaka 50, TET inatarajia kufanya shughuli mbalimbali za kielimu pamoja na za kijamii ikiwemo Kongamano la elimu na matembezi ya hisani.
“Kuelekea miaka hamsini tumejipanga kufanya shughuli kadhaa ambazo zitahusisha kazi zetu katika jamii, tukio hilo litawajumuisha wadau wa Elimu nchini watakaojadili masuala ya Elimu, mafunzo ya walimu kazini, upandaji wa miti kwa ajili ya kutunza mazingira,” alisema Dkt. Komba.
Aidha amesema pia kutakuwa na matembezi ya hisani, ili kupata pesa za kuandaa vitabu kwaajili ya wanafunzi viziwi, huku akiwaomba wadau wa elimu kuwaunga mkono katika kuelekea kilele cha miaka 50 ya TET.

Tumepata somo kuchunguza usalama wa Maghorofa - Rais Samia
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 21, 2024