Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi, imemuhukumu kifungo cha maisha gerezani Athuman Mohamed Mnumu (19), kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 9,
Mnunu ambaye ni mkazi wa Rutamba Wilayani Lindi, alipatikana na hatia ya kumlawiti Mtoto huyo jinsia ya kiume na Mwanafunzi wa Darasa la Kwanza.
Hukumu hiyo ya kesi namba 21707 ya mwaka 2024, imetolewa Novemba 21, 2024 na Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Delphina Kimath baada ya mtuhumiwa kukutwa na hatia.