Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Lindi, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Joyce Kitesho ameitaka jamii kutowabagua na kuwatenga Watu wenye ulemavu na usonji.
Mkaguzi Kitesho aliyasema hayo wakati akiwa anaelimisha Jamii kupitia kipindi cha Redio moja iliyopo Kata ya Mitandi Manispaa ya Lindi.
Amesema, Wananchi wanatakiwa kutowanyanyasa na kuwabagua watu wenye ulemavu na usonji lakini pia wasisite kuwafichua watu wanaowafanyia ukatili kwa kutoa taarifa mapema, ili hatua zichukuliwe haraka.
Aidha, Kitesho pia aliwataka Wananchi kulitumia Dawati la Jinsia na Watoto kupata elimu, msaada, kutoa taarifa za uhalifu na kupatiwa ushauri mbalimbali juu ya malezi bora kwa jamii, ili kuepuka kutenda makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.

Bukoba: CHADEMA waahidi huduma bure kwa Wananchi
Lindi: Mnunu jela maisha kwa kulawiti Mtoto wa Darasa la Kwanza