Viongozi wa Dini Mkoa wa Simiyu, wamehimizwa kuendelea kuhubiri amani ya nchi ili kujenga jamii iliyo bora.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi Sunday Songwe wakati akifunga Kikao cha Jumuiya ya Maridhiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Simiyu.
Amesema, Nyumba za Ibada zinatakiwa zitumike kuhubiri amani na utulivu jambo litakalosaidia waumini wa dini zote kuishi maisha ya amani na utulivu huku akuiwataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele kufichua vitendo vya uhalifu na wahalifu katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Mkoa wa Simiyu, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Glory Outreach Assembly Tanzania, Dominick Ishengoma Kabobe amesema watakuwa chachu ya kupambana na vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali.