MATOKEO YA UJUMLA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.

WANANCHI 26,963,182 WAPIGA KURA.

Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura lilifanyika kuanzia Oktoba 11-20, 2024 ambapo jumla ya wapiga kura 31,282,331 walijiandikisha. Kati yao, Wanawake walikuwa 16,045,559 na wanaume walikuwa 15,236,772.

Aidha, kwa mujibu wa kanuni ya 12 ya Tangazo la Serikali Na. 571, 573 na 574 na Kanuni ya 11 ya Tangazo la Serikali Na. 572 kulikuwa na muda wa wananchi kuweka pingamizi kwa Wananchi waliojiandikisha.

Baada ya kushughulikia pingamizi wapiga kura waliohakikiwa kwa ajili ya kupiga kura walikuwa 31,255,303.

Pingamizi za uandikishaji zilitokana na sababu mbalimbali ikiwemo wananchi kutokuwa wakazi wa maeneo husika na wengine kujiandikisha kwenye maeneo wanayofanya shughuli zao za kiuchumi badala ya maeneo yao ya makazi.

Aidha, Wananchi waliopiga kura siku ya Novemba 27, 2024 ni 26,963,182 sawa na asilimia 86.36 ya wananchi waliokuwa na sifa ya kupiga kura.

1. Nafasi za Mwenyekiti wa Kijiji.

Nafasi zilizogombewa ni 12,271 kati ya nafasi 12,280 zilizopaswa kufanya uchaguzi.

● CCM imeshinda nafasi 12,150 sawa na asilimia 99.01

● CHADEMA imeshinda nafasi 97 sawa na asilimia 0.79

●ACT Wazalendo imeshinda nafasi 11 sawa na asilimia 0.09

●CUF imeshinda nafasi 10 sawa na asilimia 0.08

● NCCR Mageuzi imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01

●UMD imeshinda nafasi sawa na asilimia 0.01

● ADC imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01

Aidha, vijiji 9 havikufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo vya wagombea baada ya uteuzi.

2. *Nafasi za Mwenyekiti wa Mtaa*

Nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa zilikuwa 4,264 kati ya nafasi 4,264 zilizopaswa kufanya uchaguzi.

●CCM imeshinda nafasi 4,213 sawa na asilimia 98.83

●CHADEMA imeshinda nafasi 36 sawa na asilimia 0.84,

●ACT Wazalendo imeshinda nafasi 9 sawa na asilimia 0.21,

●CUF imeshinda nafasi 4 sawa na

asilimia 0.09 na

●CHAUMA imeshinda nafasi 1 sawa na

asilimia 0.02.

Mtaa mmoja wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga hakupatikana mshindi kwa sababu kura za wagombea wawili zilifungana.

Shule za Msingi 139 Mbinga kupewa Kompyuta
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 29, 2024