Ni miaka 8 imepita tangu Simba ianze mchakato wa mabadiliko ya umiliki na uendeshaji wa timu. Mchakato huo ulianza mapema 2018 ukimhusisha Mohammed Dewji aliyepanga kununua hisa na kuimiliki klabu hiyo kwa asilimia 49 huku wanachama wakibaki na asilimia 51. Mpaka sasa mchakato huo haujakamilika na haijajulikana utakamilika lini.

Tangu wakati huo Mohammed Dewji amekuwa msitari wa mbele katika uwekezaji ndani ya Simba kuanzia ununuzi wa wachezaji na uendeshaji wake .

Mnamo mwaka 2021 Mohammed Dewji aliikabidhi klabu ya Simba chini ya mwenyekiti Muktadha Mangungu hundi ya shilingi bilioni 20 kama manunuzi ya hisa kwa asilimia 49 na aliahidi kuendelea kuwekeza ndani ya klabu hiyo ikiwemo ujenzi wa uwanja ,gym na kambi lakini hayoo yote yanashindikana kwa sasa kwa sababu hati ya umiliki haijatolewa mpaka sasa kutoka RITA.

Taarifa zisizo rasmi zinasema kwamba shirika la kiserikali la RITA (Registration Insolvency  and Trusteeship Agency ) linakwamisha  mabadiliko ya mfumo kwa klabu ya Simba. Chanzo kisicho rasmi na kilichokataa kutajwa kimenukuliwa kikisema

”RITA wamekuwa wakitoa maagizo kwa vipindi kwa maana kila Simba wanapokwenda hupewa jambo jipya na wakilitekeleza wanapoliwasilisha hupewa jipya tena”

”Kwa kweli hadi tunakata tamaa sababu tunaona kuna sababu mpya kila tukienda na wakati mwingine inaonekana kama kuna ukwamishaji wa makusudi”

”Tukitekeleza agizo hili wanaibua jipya jambo ambalo linaonyesha kuna kitu si cha kawaida”kilieleza chanzo hicho

”Naona kama kuna watu ndani ya RITA hawataki mapinduzi ya mpira wa miguu ,wanataka kuua jitihada za Mh.Raisi Samia Suluhu kwenye eneo la mpira wa miguu ,inaumiza sanasana”

 

Madrid yazidi kupaa kileleni Barcelona wakidorola
Tetesi za soka duniani Disemba 2