Mabao ya Jude Bellingham dakika ya 30 kwa mkwaju wa penati na Kylian Mbappe dakika ya 38 yameifanya Real Madrid kufikisha alama 33 katika michezo 14 ya La Liga. Alama hizo zinawafanya Madrid kusalia nafasi ya pili nyuma ya vinara Barcelona wenye alama 34 katika michezo 15 waliyocheza.

Real Madrid atacheza mchezo wake wa 15 dhidi ya Athletic Club na kama ataibuka na ushindi katika mchezo huo basi atarejea kileleni kwa alama 36 akiwazidi Barclona.

Barcelona wameteleza wapi?

Barcelona walianza vyema La Liga msimu huu na ushindi mnene wa mabao 4-0 walioupata dhidi ya Real Madrid ulizidi kuaminisha mashabiki wake kwamba wamerejea rasmi kurudisha heshima waliyoipoteza kwa miaka ya karibuni,

Kufungwa bao 1-0 dhidi ya Real Sociedad ,Sare ya 2-2 dhidi ya Celta vigo na kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Las Palmas kumeibua sintofahamu kwa wachezaji na mashabiki wa timu hiyo.Wengi wameingiwa na mashaka namna kikosi chao kinavyoshindwa kuvuna alama 3 La Liga ilihali michuano ya UEFA wanafanya vizuri.

Kesi za Uhalifu: Rais Biden amsamehe Mtoto wake
Wanaokwamisha uwekezaji wa Mo Dewji ndani ya Simba wajulikana