Kocha mpya wa Manchester United ,Ruben Amorim ameendelea kufanya vizuri baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Everton kwenye mchezo wa raundi ya 13 ya EPL. Kocha huyo ameiongoza United katika michezo katika michezo mitatu akishinda 2 na sare moja.
Tathmini ya mchezo dhidi ya Everton
Amorim aliingia na mfumo wa 3-4-2-1 na fomula hii ya ushambuliaji iliundwa na Andre Onana,,Mazraoui,De Ligt na Martinez kwa eneo la ulinzi.Eneo la kiungo liliundwa na Amad Diallo,Mainoo,Casemiro na Dalot na washambuliaji wakiwa ni Rashford ,Bruno Fernandes na Zirkzee .
Marcos Rashford ndiye aliyefungua akaunti ya mabao dakika ya 34 na Zirkzee aliweka bao la pili dakika ya 41 na kufanya mchezo kwenda mapumziko United wakiongoza kwa mabao 2-0.
Dakika ya 46 Marcus Rashford alirejea tena langoni mwa Everton na kuandika bao la tatu .Dakika ya 64 Zirkzee alirejea tena langoni mwa Everton na kuandika bao la nne na kukamilisha ushindi mnono kwa United.
Matokeo hayo yanawafanya United kufikisha alama 19 katika michezo 13 waliyocheza na wameshika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa ligiwakifunga mabao 17 na kuruhusu 13