Swaum Katambo – Katavi.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda amekabidhi jumla ya hati miliki za kimila 350 kwa wananchi wa Kijiji cha Ikulwe kilichopo Kata ya Majimoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi.

Tukio hilo la ugawaji wa hatimiliki za kimila limefanyika katika mkutano wa kijiji uliohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Mpimbwe Shamim Mwariko.

Pinda amewataka kuhakikisha hati miliki hizo hawazitoi kwa mtu yeyote kwani ni nyaraka za siri ambayo itamwezesha mwananchi kama dhamana ya kuaminiwa kupata mikopo kupitia taasisi za kifedha

Aidha amewataka wananchi wa Ikulwe kutunza hatimiliki hizo sehemu salama ili zisiharibike na maji.

 

Kadhalika, amewahakikishia wananchi kuwa hati hizo zitaenda kupunguza migogoro ya ardhi baina yao kwa kuwa zoezi la utambuzi wa maeneo na uwekaji alama za msingi limefanyika na wananchi kupatiwa hati.

Kwa upande wao wananchi waliopokea hati hizo wameshukuru kupatiwa hati hizo huku wakidai kuwa hatimiliki hizo ndio mwarobaini wa migogoro ya ardhi ilikuwa ikitokea.

Kesi ya ukatili: Gekul afunguka kwa mara ya kwanza
Demo Sugar Rush Pragmatic Oyna