Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Mbunge wa CCM Jimbo la Babati Mjini Mkoani Manyara, Pauline Philipo Gekul kwa mara ya kwanza amezungumza na kukanusha vikali kutohusika na tuhuma za kufanyiwa vitendo vya ukatili kijana Hashim Ally.

Gekul amezungumza hayo mbele ya Waandishi wa Habari pamoja na Wananchi wa Jimbo la Babati Mjini, waliohudhuria hafla yake ya kutoa shukrani kwa Mungu Mkoani Manyara na kusema tukio hilo ni la kutengenezwa, ili kumchafua.

Amesema, baada ya vipimo vya kitabibu vilivofanyika kwa kijana Hashimu Ally cheti cha Daktari kilithibitisha kuwa kijana huyo hakufanyiwa vitendo vya udhalilishaji kama ambavyo alikuwa akijieza.

“Daktari aliandika Kno any bruises, kno injuries, hakuna jeraha lolote huko ambacho chupa zilitumika kuhifadhia, huko ndani hakupata jeraha, no injuries maana siwezi kutamka nadhani mmenielewa na baadae mtasoma Waandishi,” alibainisha Gekul.

Ameongeza kuwa, “mimi sikufanya ukatili, lakini nchi hii wenye kufanya makosa mkubwa makubwa Jamhuri ndo inamshitaki mtu huyo aliefanya makosa na sio tu mtu wa kawaida, wale walioondoka kwenye kushitaki Mahakamani, Mahakama ilisikiliza na kuendelea na taratibu zake.”

Awali, aliungana na waumini wa Kanisa la KKKT kutoa shukrani kwa Mungu kwa magumu aliyoyapitia huku akiongoza harambee ya uchangiaji wa fedha ili kumalizia ujenzi wa kanisa hilo ambapo Shilingi milioni 116 zilipatikana huku fedha tasilimu zikiwa ni Shilingi milioni 90.

Nao, baadhi ya Viongozi wa Dini waliohuduria hafla hiyo wametoa msisitizo kwa Wananchi kuona umuhimu wa kumtukia Mungu katika nyakati zote ngumu na za furaha na kutumia fursa hiyo pia kuwaombea Viongozi wa Serikali waweze kufanya kazi zao kwa uadilifu na uaminifu na kuzingatia maadili ya kazi, huku wakimtia moyo Mbunge huyo kuendelea kumuamini Mungu.

“Mitihani,majaribu hayo ni mambo ya kawaida katika maisha ,dhahabu lazima ipite kwenye moto lakini sisi tunaangalia dhahabu tu,na Hilo kushukuru mungu usiangalie kama uliumia wewe shukuru tu,sisi tunaangalia jinsi mungu alivokuasaidia,” alisema mchungaji Jasson Kahembe.

“Mtihani uliomkuta akaona amlilie Mwenyezi Mungu muumba wa viumbe wote,na kwasababu limepita kwa kheri akaamua kufanya hivi,hii ndo ishara ambayo amefanya anamshukuru mungu juu yake kwa uwezo wake,na siku zote muegemee sana Mwenyezi Mungu kwa Kila kitu na iwe darasa kwa Kila mmoja,” aliongeza Sheikh Hamis Ramadhan.

Saba wafariki Dunia kwa ajali Kagera
Hati ya ardhi haiazimishwi - Pinda