Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA ) wakishirikiana na Benki ya Dunia, wamekaa kikao cha Mkakati na Wafanyabiashara wa ndani ili kujadili namna bora ya kutumia fursa zilizopo katika sekta ya Ununuzi wa Umma kwa Wafanyabiashara wa ndani.

Kikao hicho kilichofanyika Desemba 4, 2024 Jijini Dar Es Salaam, kimehudhuriwa na Wafanyabiashara zaidi ya 70 kutoka Tanzania bara na Visiwani.

Mgeni rasmi wa kikao hicho, ni Naibu katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Elija Mwandumbya amesema kuwa kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuitaka Wizara kuketi pamoja na Wafanyabiashara wa ndani ili kujadili Mustakabali wa maendeleo katika sekta husika Nchini.

“Sisi kama Serikali, kwa niaba ya Wizara ya Fedha napenda niahidi kuwa tutashirikiana nanyi muda wote, ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu, lakini pia najua mnatambua mchango wa wenzetu.

Tetesi za soka Duniani Disemba 06
hello world