Afarah Suleiman, Simanjiro – Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mwl. Fakii Lulandala ameshiriki maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kupanda miti na kufanya Usafi katika Taasisi mbalimbali za Serikali na Soko kuu la Orkesument Wilayani humo.
Akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo, Mwl. Lulandala ametoa maelekezo ya shughuli hizo kiwa ziwe endelevu kwenye Wilaya hiyo na sio kwa siku za matukio maalum pekee.
Shughuli hizo za upandaji wa Miti na Usafi wa Mazingira ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Wilaya na Mikoa yote Nchini katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru mwaka huu 2024.