Viongozi wa Serikali ya Mtaa wametakiwa kushirikiana nq Polisi kata kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi, ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao, huku akiwasihi kutunza siri za uhalifu na si kuzitoa kwa marafiki au wenza wao.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Wa Polisi, George Katabazi katika mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Kikuyu Magengeni.

“Epukeni kutoa malalamiko bila kutimiza wajibu, suala la ulinzi na usalama katika jamii ni la jamii nzima, tushirikiane kwa pamoja mtoe taarifa za wahalifu nasisi tutawashughulikia kwa mujibu wa sheria,” alisema Kamanda Katabazi.

Aidha, Katabazi amesema pindi mnapotoa taarifa za siri za wahalifu mfanye kuwa siri na kuacha kutangaza kwa marafiki, vijiweni na hata kwa wenza wenu kwani kuna dawati la jinsia, namba za Simu za viongozi wa Jeshi la Polisi ili kudhibiti uhalifu.

Hata ivyo katabazi amekemea vitendo vya matumizi ya dawa za kulevya, unywaji wa pombe kiholela muda wa kazi, kujichukulia sheria mkononi kwa wahalifu na kusababisha mauaji ambalo ni kunyume na Sheria.

Mkutano huo ulifanyika katika Kata ya Kikuu Magengeni ni muendelezo wa ziara ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma akiambarana na watendaji wa Jeshi la Polisi Dodoma kusikiliza kero za wananchi juu ya ulinzi na usalama.

G7: Tutasaidia mchakato kipindi cha mpito Syria
Serikali kuendeleza utatuzi changamoto za Walimu