Mwanamke mmoja, Neema Wikechi (21), mkazi wa Idundilanga Halmashauri ya mji wa Njombe anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumjeruhi vibaya Mume wake Flowin Msigwa (27), kwa kumkata na kitu chenye makali sehemu za siri kisa wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga amesema tukio hilo lilitokea Novemba 25, 2024 na kusema majeruhi amepatiwa matibabu afya yake inkiendelea kuimarika, huku mtuhumiwa akitarajiwa kufikishwa Mahakamani.
Amesema, “lakini sababu kubwa ya tukio hili ni ugomvi katika familia kwenye maswala mazima ya wivu wa mapenzi kwasababu Mwanaume ana Mwanamke mwingine ambaye anaishi naye.”
Kufuatia tukio hilo, Kamanda Banga ametoa wito kwa Wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuwasihi kuendelea kushirikiana na Polisi katika utoaji wa taarifa, ili kukabiliana na uhalifu na wahalifu.