Johansen Buberwa – Kagera.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika tamasha la Ijuka Omuka litakalofanyika mkoani Kagera kwa siku tisa likiambatana na shughuli mbalimbali za maonesho lenye lengo wa kuwavutia wawekezaji kuwekeza ndani ya Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa Kagera, Hajjat Fatma Mwasa amezungumza na Vyombo vya Habari Ofisini kwake na kusema Tamasha hilo la pili litakalo anza Desemba 18 hadi 26, 2024 likiwa limekidhi matakwa, mahitaji na utashi wa kila mmoja.
Amesema, “Tarehe 18 itaanza dua ya kuombea mMkoa, Taifa pamoja na Mhe, Rais Samia Hassan na siku hiyo maonesho ya Biashara yatazinduliwa katika Viwanja vya CCM Manispaa ya Bukoba na Tarehe 19 litakuwepo Kongamano la Biashara na Watendaji wa Serikali, ili kuondoa changamoto zote za kibiashara zinazowakabili.”
“Siku hiyo hiyo mchana litakuwepo tamasha la utamaduni wa mtu wa Kagera ndani ya uwanja wa Katabazi na usiku wake kutakuwepo garadina,” amesema Hajjat Mwasa.