Hatimaye michuano ya DAR24 Chandimu Cup imeanza rasmi wilayani Temeke Jijini Dar es salaam katika viwanja vya Msufini ikiwakutanisha Magogo FC dhidi ya 770 FC. Mchezo huo wa ufunguzi uliokuwa na ushindani mkali kwa pande zote mbili ulimalizika kwa kishindo baada ya  770 FC kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 .

Magogo yapoteza mchezo

Kikosi cha Magogo fc  kilichoundwa na Para,Ally,Rashid,Banda,Uchebe,Felix, River ,Haland ,Jazir na Elisha na kunolewa na kocha John kilianza kwa kasi na dakika ya pili ya mchezo kilipata bao la uongozi lililowekwa kimiani na Felix. Bao hilo halikudumu baada ya Shingo wa 770FC kusawazisha bao hilo na Mbumba kuongeza mabao 3 (Hat trick) na kuwafanya Magogo FC Kwenda mapumzikoni wakiwa nyuma kwa mabao 4-1.

Kipindi cha pili Magogo FC waliwapa nafasi Abdul Karim,Shimi,Salum ,Ndevu na Kuimbo .Mabadiliko hayo hayakuzaa matunda kwani mchezo ulimalizika kwa kipigo cha mabao 4-1

770 yasonga Nusu Fainali

Ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Magogo FC umewapeleka 770 FC hatua ya nusu fainali ya DAR24 Chandimu Cup. Kikosi kilichoipa timu hiyo ushindi kiliundwa na Dastan,Mtunyungu,Kapombe,Muddi Mpemba,Omary Omary,Shingo,Ally Sako,Hamis Masai,Mbumba na Kimbu. Kipindi cha pili kikosi hicho kilifanya mabadiliko kwa kuwapa nafasi Osama,Jabia,Kinje,Shengoma na Demba.

770 FC watamngojea mshindi kati ya Mzinga FC au Videte Academy katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea dimba la Msufini Chamazi

MBUMBA Kinara wa Magoli

Mabao matatu yaliyowekwa kimiani na mshambuliaji Mbumba wa 770 fc yanamfanya nyota huyo kuwa kinara wa ufungaji akifuatiwa na Shingo pamoja na Felix wote wakiwa na bao 1. Mbali na mabao hayo Mbumba ndiye aliyeibuka kuwa nyota wa mchezo huo wa robo fainali.

 

 

Papa awaonya Makasisi kuacha kufanya Siasa
Byabato atumia Bukoba Mjini Mpya Festival kuwafariji Watoto yatima