Kupitia ukirasa wake wa X, Makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu ameandika kuwa Watu wasiojulikana wanapanga njama za kumuumiza kisha wamsingizie Mwenyekiti wake Freeman Mbowe.

Lissu ambaye pia ni Mgombea Uenyekiti wa Chama hicho, katika andiko lake hilo alilolichapidha hii leo Desemba 16, 2024 ameeleza kuwa amezisikia njama za watu hao na kudai kuwa wamekuwa wakiwaumiza watu wasio na hatia.

Ameeleza kuwa, “enyi Watu wabaya mjulikanao kama ‘Watu wasiojulikana,’ nimezisikia njama zenu, mnataka kuniumiza halafu mumsingizie Mwenyekiti wetu wa Chama, Freeman Mbowe, ndivyo mlivyofanya wakati wa kifo cha marehemu Chacha Wangwe.”

Andiko hilo linaendelea kueleza kuwa, “ndivyo mlivyofanya tena wakati mliponishambulia tarehe 7 Sept ‘17 na ndivyo mlivyofanya miezi michache iliyopita mlipomteka nyara na kumuua Mzee Ali Mohamed Kibao.”

Lisu anaeleza zidi kwamba, “ndivyo mavyofanya kila mnapoua Watu wasio na hatia, mnasingizia Watu wengine ili nyie mnaohusika msiwajibike na udhalimu wenu, huyo mnayedhani mnamtumikia alitoa ahadi hadharani kuwa nitakuwa salama nikirudi nyumbani, Waziri wake Masauni alirudia ahadi hiyo Bungeni.”

“Mkiniumiza kama mnavyopanga mjue lawama yote itaangukia kwa Samia Suluhu Hassan badala ya kumlinda mtamchafua zaidi na kama ilivyokuwa kwa Magufuli baada ya 7 Sept ‘17, ndivyo itakavyokuwa kwa Samia,” amekamilisha andiko lake Lissu.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 17, 2024
Dkt. Biteko: Kuna umuhimu wa kuwawezesha Wabujifu wetu