Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka, 2025 umezingatia kigezo cha ufaulu wa mtahiniwa anayechaguliwa.
Kila mtahiniwa aliyefanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka, 2024 na kupata jumla ya alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300 amechaguliwa na kupangiwa Shule ya Sekondari ya Serikali.
Uchaguzi huu umehusisha wanafunzi 974,332 sawa na asilimia 100 ya wanafunzi wote waliokuwa na sifa ya kuchaguliwa wakiwemo Wasichana 525,225 na Wavulana 449,107.
Wanafunzi hao ni wale waliofanya na kufaulu Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka, 2024.
Waliofaulu wapangiwa Shule
Shule za Sekondari za Serikali walizopangiwa wanafunzi zipo katika makundi mawili ambayo ni Shule za Bweni na Shule za Kutwa.
Shule za Sekondari za Bweni za Serikali zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni; Shule za Sekondari za Bweni za Wanafunzi wenye ufaulu wa Juu (Special Schools), Shule za Amali za Kihandisi (Ufundi) na Bweni Taifa.
Shule za Bweni ni za Kitaifa hivyo, zimepangiwa Wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuzingatia mgawanyo wa nafasi uliobainishwa na vigezo vilivyowekwa ili kuimarisha Utaifa