Wananchi wa Kijiji cha Misinko Kata ya Ughandi Wilaya na Mkoa wa Singida, wamesisitizwa kutunza mazingira yao katika kipindi hiki cha mvua ili kujilinda dhidi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Hayo yameelezwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Lucas Makaya ambaye ni Mkaguzi Kata ya Mtinko alipokuwa akitoa elimu kwa Wananchi katika Zahanati ya Kijiji cha Msinko, Tarafa ya Mtinko Wilaya na Mkoa wa Singida.
Aidha, Makaya amewataka wananchi hao kutojichukulia sheria mkononi badala yake watoe taarifa na uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi, ili hatua za kisheria ziweze kufuatwa.