Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amesema atafanya mazungumzo na Viongozi wa Ukraine na Urusi ili kumaliza umwagaji damu usiomithilika kutokana na vita vya karibu miaka mitatu baina ya nchi hizo mbili.

Akizungumza kwa mara ya kwanza na Waandishi Habari tangu alipochaguliwa kwa mara nyingine kuwa rais wa Marekani, Trump amesema ni lazima mauaji yanayotakana na vita hivyo yakomeshwe.

Amesema, “tutazungumza na Rais Putin, na tutazungumza na wawakilishi, Zelensky na wawakilihsi wa Ukraine. Ni lazima tukomeshe vita, haya ni mauaji yasiyoelezeka.”

Kwa mara kadhaa, Trump amekuwa akidai anao uwezo wa kumaliza mzozo wa Ukraine haraka, licha ya kuwa hadi sasa hajaweka wazi mkakati wake.

Tetesi za Soka Duniani Disemba 17
Tutunze Mazingira kuepuka magonjwa ya mlipuko - Makaya