Jumla ya Wanafunzi 809 wakiwemo wasichana 329 na wavulana 480 wamechaguliwa kujiunga katika Shule za Sekondari za vipaji maalum.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema Sekondari hizo ni zile ambazo hupokea Wanafunzi wenye ufaulu wa Alama za Juu.
Amesema, nafasi katika Shule za Wanafunzi wenye Ufaulu wa Juu zimegawanywa kwa kila Mkoa kulingana na idadi ya watahiniwa wa Darasa la Saba waliotahiniwa katika Mkoa husika kwa kutumia Kanuni ya kugawa nafasi hizo Kitaifa.
Nafasi zilizotolewa kwa Mkoa zimegawanywa sawa kwa Halmashauri zote bila kujali idadi ya watahiniwa waliotahiniwa katika Halmashauri ambapo Shule hizo ni Ilboru, Msalato, Kibaha, Kilakala, Mzumbe, Tabora Boys na Tabora Girls.