Kilimo ni uzalishaji wa mazao kwenye mashamba lakini kimebeba maana kubwa na pana inayojumuisha mifumo mbalimbali.

Mifumo hiyo ni ya uzalishaji mimea, ufugaji wa wanyama na uvuvi wa samaki, ingawa mara nyingi Kilimo cha mimea huenda sambamba na ufugaji wa wanyama.

Kiuhalisia Watu hupanda mimea na kuitunza hadi wakati wa mavuno hasa kwa uzalishaji wa chakula cha binadamu na lishe ya wanyama.

Aidha, Kilimo hutumiwa pia kwa shabaha ya kupata malighafi za mazao mbalimbali ikiwemo Pamba zinazotumiwa kwa kutengeneza mavazi yanayovaliwa na watu.

Siku hizi kilimo kinalenga pia nishati ya mimea na ifahamike kwamba Mtu anayejihusisha na kilimo huitwa Mkulima.

Ulega ataka kasi ya Kijeshi Miradi ya dharura TANROADS
Afya: Uvutaji Sigara wa mapema hupelekea magonjwa ya Moyo