Takriban Watu 38 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 hawajulikani walipo nchini Kongo, baada ya kivuko walichokuwa wakisafiria kilichozidisha mzigo kupinduka katika mto Busira, wakati wakirudi nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya Krismasi.

Meya wa mji wa Ingende ulio mwisho kabla ya eneo la ajali, Joseph Kangolingoli alisema wengi wa abiria waliokuwa katika kivuko hicho walikuwa ni Wafanyabiashara na walikuwa wakirudi nyumbani kwa mapumziko ya sikukuu hiyo.

Tukio hili linatokea chini ya siku nne baada ya boti nyingine kupinduka kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 25 na inaarifiwa kuwa licha ya Maafisa wa Kongo kuonya mara nyingi dhidi ya kuzidisha mzigo, lakini, wengi wa abiria hawawezi kumudu usafiri wa umma.

Ikumbukukwe kuwa Watu wengine wasiopungua 78 walikufa maji Oktoba 2024 wakati boti iliyozidisha mzigo ilipozama mashariki mwa nchi hiyo, huku watu 80 wakipoteza maisha katika ajali kama hiyo karibu na Kinshasa Juni 2024.

Dkt. Kazungu atembelea Miradi ya Umeme Dar es Salaam
IGP afanya mabadiliko madogo Usalama Barabarani