Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kwenye Ofisi ya Msajili na Hazina, Amos Nnko na binti yake Maureen Nnko wamefariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea Wilayani Same, mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu imeeleza kuwa ajali hiyo iliyotokea Desemba 22, 2024 majira ya mchana.
Taarifa hiyo pia imefafanua kuwa mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina.”
Katika ajali hiyo, mke wa marehemu na watoto wengine wawili na mwanafamilia mmoja walijeruhiwa na wanapatiwa matibabu katika hospitali za KCMC na Mawenzi Mkoani Kilimanjaro.