Wazazi na walezi ametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo vya ukatili na Unyanyasaji wa watoto, ili kutokomeza vitendo hivyo viovu na kuleta amani na utivu katika jamii.

Wito huo umetolewa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Ramadhan Duru hii leo Desemba 24, 2024 alipoambatana na Koplo wa Polisi (CPL) Festa Kayombo wa Kituo cha Polisi Peramiho cha Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.

Kwa pamoja walikuwa wakitoa elimu ya ushirikishwaji jamii katika kituo cha kuelelea Watoto wanaoishi katika mazingira magumu kinachomilikiwa na Kanisa la Pentekoste Tanzania – KLPT, kilichopo Lundusi Peramiho katika halfa fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya Watoto kuelekea Sikukuu ya Krismasi.

Aidha, wazazi pia wametakiwa kutokuwa wakali kupitiliza kwa Watoto na badala yake wawe karibu nao, ili kutambua changamoto mbalimbali hasa za vitendo vya ukatili vinavyowakabili na kuzipatia ufumbuzi kabla ya kuleta madhara.

Kwa upande wao watoto, wao wametakiwa kuepuka kujiingiza kwenye makundi mabaya yanayojihusisha na vitendo viovu ikiwemo udokozi, utoro shuleni, kujihusisha na mapenzi ya utotoni kwani ni kinyume na maadili hivyo wazingatie masomo.

Tabora: Mwl. Doto Jela maisha kwa kubaka mtoto
Maisha: Bet yampa utajiri baada ya kutapeliwa