Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, imemuhukumu kifungo cha maisha Mwl. Dotto Masatu wa Shule binafsi ya awali na msingi ya St. Doroth kwa kukutwa na hatia ya kumlawiti mwanafunzi mwenye umri wa miaka minane.

Mbali na kifungo hicho, pia Mwl. Doto ambaye alifanya kitendo hiko kwa Mwanafunzi huyo anayesoma katika shule yake, pia atatakiwa kulipia fidia ya Shilingi 500,000/=

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Sigwa Mzige amesema Mahakama imepitia ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha pasi na shaka na kumkuta na hatia mwalimu huyo.

Dotto Masatu anadaiwa kutenda kosa hilo akiwa shuleni nyakati za mapumziko katika tarehe tofauti tofauti kuanzia Mei hadi Julai 2024, kinyume na kifungu cha sheria cha 154 kidogo cha kwanza na cha pili.

Kinywaji cha Mbulungo kilivyouwa 50 kwa mpigo
Wazazi watakiwa kuwalinda Watoto dhidi ya vitendo viovu