Mti huu wa Mbuyu, unadaiwa kuwa na umri wa miaka 1,500 ukiwa na urefi wa mita 22 sawa na futi 72 na upana wa mita 10.64 ambazo ni sawa na futi 34.9.
Mbuyu huu uliopo Kusini mwa Bara la Afrika wanauita “Mti wa Uzima” upo Sunland Farm huko Limpopo Nchini Afrika Kusini.
Una shina kubwa, matawi yanayotanuka na mwonekano wa kipekee wa juu na chini ukiwa ni mojawapo ya miti hai ya kale zaidi duniani.