Watu wanne wamefariki na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia kupigwa na shoti ya umeme baada ya hema walilokalia kugusana na nyaya za umeme wa line kubwa wakiwa msibani katika Mtaa wa Ngugwini, Halmashauri ya Mji wa Handeni mkoani Tanga.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi imeeleza kuwa tukio hilo limetokea hii leo Desemba 24, 2024 majira saa 3:40 asubuhi katika mtaa huo.
Taarifa hiyo imewataja waliofariki katika tukio hilo kuwa ni Fredy William Mwangunda (43), Mhina Athuman Mangagwa (35), Andrew Allen Mkomwa (29) na Salehe Omary Machaky (25) huku majeruhi wakiwa ni William Gumbo (50) na Mbega Ally (49).