Ibada ya mkesha wa Krismasi katika Wilaya ya Serere Nchini Uganda, iligeuka kuwa majanga kufuatia Muumini mmoja mwenye pepo kumpiga teke Mchungaji John Michael Ekamu (52), na kupelekea kifo chake wakati wa akijaribu kumtoa pepo.

Polisi aliyeripoti taarifa hiyo, Joseph Erutu amesema tukio hilo lilitokea katika Kanisa la Agule Pentecostal Assemblies of God (PAG) lililopo Kijiji cha Ocuko cha Parokia ya Omagara Kata ndogo ya Kateta, Wilayani humo.

Marehemu, John Michael Ekamu, 52, alikuwa Mchungaji wa Kanisa hilo la Agule PAG na ni mkazi wa Kijiji cha Osokotoit kilichopo katika Kaunti Ndogo ya Kateta na alipigwa teke hilo na Mshukiwa Osagani Simon Ogwang (30), wa Kijiji cha Mutebe, Parokia ya Omagara.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kyoga Mashariki, Damalie Nachuha.

Inaarifiwa kuwa, aliwasili Kanisani hapo akitokea jijini Kampala Desemba 24, 2024 ambapo alipelekwa na baba yake Mzee Ogwang, ili afanyiwe maombi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kyoga Mashariki, Damalie Nachuha alisema Baba yake Osagani alidai kuwa mwanawe alishambuliwa na mapepo na wakati wa maombi ndipo alimpiga teke Mchungaji Ekamu, ambaye alianguka na kufariki baadaye.

Tayari mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Seroti kwa ajili ya uchunguzi mara baada ya kufanyiwa vipimo vya upasuaji.

Ajali Basi la Ngasere, Noah yauwa Tisa Rombo
RC Mwasa asherehekea Sikukuu na Watoto, Wanahabari wajumuika