Jeshi la Polisi Nchini Kenya, limekanusha madai ya kuhusika na visa vya utekaji unaowalenga wakosoaji wa Serikali, huku ikidaiwa Watu 74 walitekwa tangu maandamano ya kuipinga Serikali kuanza na 26 kati yao bado hawajulikani walipo.

Taarifa ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini humo, Douglas Kanja imweleza kuwa imeshtushwa na madai yanayoendelea kwamba Maafisa wa Polisi wanahusika na utekaji wa watu.

Hatua hiyo inakuja baada ya Vikosi vya usalama vya Kenya kutuhumiwa na mashirika kadhaa ya haki za binadamu kwa kuwateka na kuwaweka kizuizini kinyume cha sheria watu tangu maandamano makubwa ya kuipinga serikali ya Juni na Julai 2024.

Hata hivyo, wakati Polisi ikikanusha madai hayo, bado haijasema kama imepiga hatua kiasi gani katika kuwatambua wanaohusika na utekaji huo.

Tume ya Kitaifa ya Haki za Binaadamu ilisema mapema mwezi huu kuwa karibu watu 74 walitekwa tangu maandamano ya kuipinga serikali, huku 26 wakiwa bado hawajulikani waliko.

Afya Tip: Papai linavyowatibu wengi bila kufahamu
Majaliwa akabidhi Tuzo kwa Wadau wa Masumbwi Nchini